Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Brazil na FAO wasaini makubaliano ya kuzipa msaada nchi zinazozalisha pamba

Brazil na FAO wasaini makubaliano ya kuzipa msaada nchi zinazozalisha pamba

Taifa la Brazil pamoja na shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO wametia sahihi makubaliano ya ushirikiano wa Kusini- Kusini wenye gharama ya dola milioni 20 yaliyo na lengo la kutuma utaalamu kuhusu pamba kutoka nchini Brazil kwenda nchi zingine zinazoendelea.

Ushirikiano huo wa miaka minne kati ya FAO na taasisi ya pamba nchini Brazil utalenga nchi zinazoshiriki na kuzipa msaada wa kiufundi kwenye kilimo cha pamba na kwenye mauzo. Mradi huo utaangazia kwanza taifa la Haiti na eneo la MERCOSUR la Amerika Kusini na kupanuliwa baadaye kwenda nchi zingine zinazoendelea sehemu za Amerika kusini na Afrika. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)