Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chama cha ITU chazindua mipango ya kuchangia maendelo endelevu

Chama cha ITU chazindua mipango ya kuchangia maendelo endelevu

Chama cha kimataifa cha mawasiliano ITU kimezindua mipango miwili mipya yenye malengo ya kuboresha teknolojia ya mawasiliano hasa mawasiloano ya matandao kipitia simu za mkononi. Mipango hiyo miwili inayojulikana kama m-Powering Development na Smart Sustainable Development Model ilinzinduliwa mwaka 2012 na sasa iko kwenye maonyesho mjini Dubai.

Chama cha ITU kinalenga kuboresha teknolojia na mawasiliano ili kuafikia maendeleo endelevu. Huku idadi ya wanaomiliki siku za mkononi ikipita watu bilioni 6 kote duniani na matumizi ya mawasilano ya simu yakiongeza , kunaweza kukawa na fursa nyingi zikiwemo za kuboresha afya, elimu , kilimo na bishara.