Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usumbufu wa akili ni tatizo la kimataifa: Ban

Usumbufu wa akili ni tatizo la kimataifa: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema usumbufu wa akili ni tatizo la kimataifa, katika ujumbe wake wa siku ya afya ya akili duniani, ambayo huadhimishwa kila Oktoba 10.

Takriban watu milioni 350 wenye umri, vipato na uraia mbali mbali, wana usumbufu wa akili, na kwamba mamilioni ya wengine, ambao ni jamaa, marafiki na wafanyakazi wenza, huathiriwa kwa njia moja au nyingine na athari za tatizo hilo la kimataifa ambalo limepuuzwa, amesema Ban.

Bwana Ban amesema usumbufu wa akili huwapunguzia watu uwezo wa kukabiliana na changamoto za maisha za kila siku, na huchangia mivutano katika familia, huharibu elimu, hufanya watu kupoteza ajira, na hata wengine kujiua unapokithiri. Amesema takriban watu milioni moja hujiua kila mwaka, hususan kutokana na usumbufu wa akili ambao haukutambulika au kutibiwa. Joshua Mmali na taarifa kamili.

(TAARIFA YA JOSHUA MMALI)