Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Udhibiti wa usalama wa mitandao ya kompyuta usiminye uhuru wa kujieleza: UNESCO

Udhibiti wa usalama wa mitandao ya kompyuta usiminye uhuru wa kujieleza: UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO limesema hatua zozote za kudhibiti usalama katika mitandao ya kompyuta duniani zisitumike kuminya uhuru wa kujieleza kwa watumiaji wa mitandao hiyo.

Hiyo ni kauli ya Mkurugenzi wa kitengo cha masuala ya uhuru wa kujieleza na maendeleo ya vyombo vya habari katika UNESCO, Guy Berger aliyotoa katika mkutano uliojadili mawasiliano baina ya watu kupitia mitandao ya kompyuta huko Budapest, Hungary.

Amesema vitisho dhidi ya uhuru wa kujieleza ni tatizo kubwa zaidi duniani kuliko matumizi mabaya ya uhuru huou ambapo amesema katika kipindi cha miaka kumi iliyopita kuminywa kwa uhuru wa kujieleza kumesababisha vifo vya waandishi wa habari 500 duniani kote.

Berger amesema usalama katika mitandao ya kompyuta na kuaminiana vitawezekana katika ulimwengu ambao watu wote wako huru kujieleza bila woga.