WHO yasisitiza umuhimu wa chanjo kwenye siku ya Kichaa cha Mbwa duniani

28 Septemba 2012

“Chanja mbwa, uokoe maisha” huu ni ujumbe kutoka Shirika la Afya Duniani ( WHO ), katika kuadhimisha siku ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa duniani, leo septemba 28.

Takriban watu elfu hamsini na tano wanapoteza maisha kwa mwaka barani Asia na Africa kutokana na homa ya mbwa, ambayo ina sambazwa kutokana na kuumwa au ku kwaruzwa na mbwa aliye na ugonjwa huu.

Dr. Francois- Xavier Meslin ni afisa wa idara ya kuzuia magonjwa ya kitropiki katika Shirika la Afya Duniani ( WHO ) mjini Geneva

Watu walio na ugonjwa wa kichaa cha mbwa hupoteza maisha kwa kasi. Hawalazwi hospitalini wala hauna tiba. Watu hufa na kuzikwa haraka. Ugonjwa huu hautambuliki haraka lakini unaweza kuzuiwa kwa chanjo. Tuna vifaa vya kukabiliana na ugonjwa huu. Tunaweza kufuta ugojwa huu Katina nchi zilizoathiriwa. Tuna technologia lakini tunakosa dhamira, kwa sababu ugonjwa huu hauonyeshi dalili yoyote”

Dalili ya ugonjwa huu ni homa kali, ugumu wakati wa kumeza au kupooza.

WHO imesema watu hufa kutokana na maumivu makali chini ya wiki moja, ingawa dalili ya ugonjwa inaweza kuenedelea kuonekana kwa muda wa wiki nane.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter