IOM kuwafunza maafisa uhamiaji, Kusini mwa Afrika, Afrika Mashariki
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM litaanzisha mafunzo ya wiki mbili yenye shabaha ya kukabiliana na wimbi la wahamiaji haramu ambao wanazidi kuongezeka barani afrika.
IOM imepanga kuwafunza maafisa kadhaa ambao baadaye watachukua jukumu la wakuelimisha wafanyakazi wenzio kwenye mataifa yao.
Shirika hilo limepanga kuwafunza maafisa kutoka mataifa 30 mbinu mbalimbali ikiwemo ile ya kuwadhibiti wahamiaji haramu, biashara ya magendo, na kubaini taarifa bandia.
Mafunzo hayo ambayo yanafadhiliwa na Umoja wa Ulaya, Umoja wa Mataifa na nchi za Japan na Marekani yanatazamiwa mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania.
Mafunzo hayo yatawaleta pamoja maafisa kutoka nchi za Malawi, Msumbiji, Zambia na Tanzania