Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya imepiga hatua katika kusuluhisha migororo: Rais Kibaki

Kenya imepiga hatua katika kusuluhisha migororo: Rais Kibaki

Rais Mwai Kibaki wa Kenya ameelezea maendeleo ya nchi yake katika nyanja mbalimbali katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Akihutubia mkutano wa 67 wa Baraza Kuu la UM Jumatano, Rais Kibaki amesema kuwa mafanikio yamekuwepo ya kina, na misingi imewekwa ya kusuluhisha migogoro kupitia njia ya amani, ikiwa ndani mwa nchi na katika kanda ya Afrika Mashariki .

Amesema, anafahamu kutokana na historia ya Kenya jirani zake, kwamba isipotatuliwa migogoro na kutoelewana kwa njia ya amani, mateso na umwagaji damu hufuata na kusababisha kuzorota kwa maendeleo ya kiuchumi na jamii, na madhara ya kutisha.

Baada ya hotuba yake Rais Kibaki ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa kuwa nchi yake imejiandaa vilivyo kwa uchaguzi ujao ili kuepukana na machafuko kama yalokuwepo mwaka 2007.  Joshua Mmali amezungumza naye kuhusu uchaguzi huo na hali nchini Somalia

(SAUTI YA MWAI KIBAKI)