Changamoto zinazoikabili sekta ya posta kujadiliwa

25 Septemba 2012

Kongamano la kimataifa kwa ajili ya kuzijadilia changamoto zinazokwaza sekta ya posta limeanza huko Doha na likiuwaleta pamoja zaidi ya wajumbe 2,000 kutoka sehemu mbalimbali.

Wajumbe kwenye kongamano hilo wanatazamia kumulika kwa kina changamoto zinazoendelea kukwaza sekta ya posta ambayo utendaji wake unaandamwa na kujitokeza na teknolojia mpya ya mawasiliano.

Kongamano hilo linaloratibiwa na Umoja wa Mataifa linatazamia kubainisha njia mujarabu zitakazosaidia sekta ya posta kupiga hatua kusonga mbele licha ya kukabiliana na ujio wa teknolojia mpya ya mawasiliano.

Mkutano huo utakaodumu kwa wiki tatu utaanisha mikakati ya pamoja ambayo pamoja na mambo mengine itasaidia kuivusha sekta ya posta.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter