Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS yaungana na Luxembourg kukabiliana na tatizo la kibinadamu Sahel

UNAIDS yaungana na Luxembourg kukabiliana na tatizo la kibinadamu Sahel

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la masuala ya UKIMWI katika Umoja wa Mataifa, Michel Sidibe, amekaribisha juhudi za taifa la Luxembourg, ambalo amesema ni mojawepo ya mataifa mengi ambayo yanajitahidi kutoa misaada katika eneo la Sahel.

Bwana Sidibe, ambaye ni raia wa Mali, amesema tatizo lililopo eneo la Sahel limeathiri vibaya eneo zima, na kwamba atafanya kila awezalo ili kulimlikia na kuchagiza juhudi za kulitatua tatizo hilo. Amesema kuna masuala mengi yasiyo rahisi kutatua yanayohusiana na tatizo hilo, akililinganisha na athari na kusambaa kwa virusi vya HIV.

Amesema, kama UKIMWI, tatizo hilo ni la kibinadam, lakini mwanzo wake ni wa kisiasa na kijamii, na watu wanaoishi na virusi vya HIV na ambao wanahitaji matibabu, wamo hatarini zaidi. Amesema anaunga mkono juhudi za taifa la Luxembourg, ambalo ni mfadhili mkubwa wa shirika analosimamia la UNAIDS.