Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikao cha 67 cha Baraza Kuu chaanza mjini New York

Kikao cha 67 cha Baraza Kuu chaanza mjini New York

Kutatua migorogo ya kimataifa kupitia njia ya amani ndio mandhari kuu ya kikao cha 67 cha Baraza Kuu la UM.

Hayo ni matamko ya Rais wa Baraza Kuu, mwanadiplomasia mkuu kutoka Serbia Vuk Jeremić katika mwanzo wa kikao hicho mjini New York Jumanne.

Amesema hakikisho la amani na usalama limejumuishwa katika Mkataba wa Umoja wa Mataifa kama lengo lake la kwanza ili kutoa nafasi kwa binadamu kuisha kwenye mafanikio makubwa.

Mheshimiwa jeremic amesema ingawa Umoja wa Mataifa hauwezi kutatua matatizo yote kwa siku moja ana uhakika kwamba Umoja huo wa Mataifa bado ni muhimu katika kukabailiana na mahitaji ya binadamu ambayo yanazidi kuongezeka.

Rais wa Baraza Kuu amesema mandhari hii inatoa uendeleaji wa kazi ya vikao vya awali na inaenda sambaba na vipaumbele vya Katibu Mkuu.

Katika wiki mbili zijazo wakuu wa dunia watakutana mjini New York kujadili masuala mbali mbali ya kimataifa.