Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wabaki wamekwama kwenye pwani ya Tunisia

Wahamiaji wabaki wamekwama kwenye pwani ya Tunisia

Kundi la wahamiaji 87 walioachwa wamekwama kwenye pwani ya Tunisia siku ya Jumapili na wasafirishaji haramu wa watu wameliomba shirika la kimataifa la uhamiaji kuwasaidia na tikiti za ndege ili waweze kurejea makwao.

Kundi hilo linawajumuisha wanawake na watoto wengi kutoka Nigeria pamoja na mataifa ya Gambia, Guniea Conakry, Guinea Bissau, Senegal, Misri, Morocco na Bangladesh. Wahamiaji hao kwa sasa wamepiga kambi kwenye makao ya chama cha mwezi mwekundu mjini Tunis wakisubiri hati za usafiri kutoka kwa balozi zao ili waweze kurudi nyumbani.

Wengi wa wakimbizi hao waliiambia IOM kwamba walikuwa wameishi nchini Libya kwa muda kabla ya kuwalipa walanguzi pesa ili wapate kuwasafirisha kwenda nchini Italia. Chris Lom ni msemaji wa IOM