Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sheria ya kimataifa inapaswa kutekelezwa bila upendeleo:UM

Sheria ya kimataifa inapaswa kutekelezwa bila upendeleo:UM

Mtaalam mpya wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuendeleza demokrasia na usawa katika utaratibu wa kimataifa, Alfred de Zayas, ametoa wito kwa mataifa kote ulimwenguni kuepukana na vizuizi vingi dhidi ya utaratibu wa kimataifa ambao ni wa kidemokrasia na usawa.

Akiwasilisha ripoti yake ya kwanza kwa Baraza la Haki za Binadamu, Bwana de Zeyas amesema kuwa shabaha hii inaweza kufikiwa kwa kuheshimu mkataba mkuu wa Umoja wa Mataifa kama mkataba wa kimataifa, kuitekeleza sheria ya kimataifa bila upendeleo, kwa kujizuia kutokana na hatari ya, au matumizi ya nguvu, na kwa kuendeleza desturi ya mazungumzo.

Amesema maendeleo ya mwanadamu ni barabara ndefu kutoka unyanyasaji hadi umoja. Mtaalam huyo huru amependekeza marekebisho katika uwanja mzima wa kimataifa, ikiwemo Baraza la Usalama, Baraza Kuu, na kusisitiza kuwa utaratibu wa kimataifa wenye demokrasia na usawa unahitaji, sio tu juhudi za kimataifa, lakini pia kuendeleza demokrasia ya kitaifa na haki ya kijamii, kupunguza pengo kati ya maskini na matajiri katika nchi zote, kuimarisha uongozi wa kisheria, uhuru wa kujieleza na taasisi huru za kisheria. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)