Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wachache zaidi wanakufa hivi sasa kabla ya kutimiza umri wa miaka mitano:WHO

Watoto wachache zaidi wanakufa hivi sasa kabla ya kutimiza umri wa miaka mitano:WHO

Kasi ya kupunguza vifo vya watoto imeongezeka kwa kiasi kikubwa tangu mwaka 2000, kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa na Umoja wa Mataifa. Ripoti hiyo inasema takriban watoto milioni saba walifariki kabla ya kutimu miaka mitano mwaka 2011, ikilinganishwa na watoto milioni 12 mwaka 1990.

Ripoti hiyo ambayo imetolewa kwa ushirikiano wa Shirika la Kuhudumia watoto, UNICEF, Shirika la Afya Duniani na Benki ya Dunia, imesema viwango vya watoto kufa vimeshuka katika maeneo yote ya ulimwengu katika miongo miwili ilopita, ingawa Kusini mwa Jangwa la Sahara bado ndilo eneo lenye kukabiliwa na changamoto kubwa zaidi katika kuokoa maisha ya watoto.

Dr Boerma Ties kutoka WHO anasema kuongeza kasi ya kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano kunawezekana kwa kupanua njia za kuzuia na kutoa matibabu ambazo zinalenga vitu vinavyosababisha vifo.

(SAUTI YA DR BOERMA TIES)

Kote duniani, kinachosababisha vifo vya watoto chini ya miaka mitano hasa ni nimonia (homa ya mapafu?) matatizo ya uzazi, kuharisha na malaria.