Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yawarejesha nyumbani wahamiaji wa Kifilipino walioko Syria

IOM yawarejesha nyumbani wahamiaji wa Kifilipino walioko Syria

Kundi la wafanyikazi wa kike 263 raia wa Ufilipino ambao walikuwa wamechukua hifadhi kwenye makao ya ubalozi wa ufilipino nchini Syria hii leo wamerejea nchini Ufilipino kupitia kwa msaada wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM. Asilimia kubwa ya wanawake waliowasili mjini Manila hii leo walikuwa ni wafanyikazi wa nyumbani wanaokimbia ghasia zinazoendelea nchini Syria.

Kupitia ombio la serikali la Ufilipino , IOM ilishirikiana kwa karibu na ubalozi wa ufilipino mjini Damascus na utawala nchini Syria ili kuwasafirisha wahamiaji hao. Tangu kuanza kwa mzozo nchini Syria mwezi Machi mwaka 2011 wafanyikazi wa kimataifa 2,150 raia wa Ufilipino wamerejea nyumbani kutoka Syria.