Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wailalamikia Ukraine kuwabana waomba hifadhi

UM wailalamikia Ukraine kuwabana waomba hifadhi

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHRC limeelezea wasiwasi wake kuhusu hali mbaya inayowaandama raia wanaoomba hifadhi ya kisiasa nchini Ukraine ambao baadhi yao sasa wanajikuta wakitupwa kizuizini.

Ripoti nyingine zinasema kuwa zaidi ya watu 100 ambao waliomba ukimbizi a kisiasa, walikataliwa na kutupwa kizuizini.

Kamishna wa UNHCR amesema kuwa ofisi yake imepokea taarifa juu ya kukamatwa kwa watu kadhaa waliokuwa wakikatiza miaka ya kimataifa na wametupwa korokoroni kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Familia nyingi zinazopita katika maeneo hayo ni zile zinazotoka katika nchi za Somalia ambako kunakosekana utengamao wa amani na ukosefu wa chakula. Pia kuna ripoti ambazo hazidhibitishwa juu ya kuwepo kwa wahamiaji kutoka nchini Afghanistan.