Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mktaba wa Kyoto wa kupunguza gesi zinazochafua mazingira wapita makubaliano bilioni moja

Mktaba wa Kyoto wa kupunguza gesi zinazochafua mazingira wapita makubaliano bilioni moja

Makubalino bilioni moja ya makataba wa Kyoto wa kupunguza gesi zinazochafua mazingira yatatolewa hii leo hatua ambayo ni muhimu katika kupunguza gesi zinazochafua mazingira dunaini. Makubaliano hayo yatatolewa kwa mradi wa kiwanda nchini India ambacho kimesitisha matumizi ya mafuta na mawe ya moto na kutumia kawi inayotokana na mimea.

Katibu mkuu kwenye mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa UNFCCC Christiana Figueres amesema kuwa mkataba wa Kyoto sio tu umeleta manufaa kwa nchi zinazoendelea lakini pia unaweza kuchochea nchi zilizostawi kuongeza malengo yao ya kupunguza gesi zinazochafua mazingira.