Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UM yaongeza jitihada za kutoa misaada Syria

Mashirika ya UM yaongeza jitihada za kutoa misaada Syria

Umoja wa Mataifa umefanyia marekebisho mahitaji yake ya ufadhili kwa ajili ya misaada ya kibinadamu nchini Syria. Umoja wa Mataifa sasa utahitaji dola milioni 347, badala ya kiwango cha awali cha dola milioni 187. Umoja wa Mataifa unasema kuwa hali ya kibinadamu Syria inaendelea kuzorota, badala ya kuimarika

Msimamizi wa operesheni za misaada ya kibinadamu, John Ging, amesema raia wa Syria wanakabiliwa na hofu na kukata tamaa, na kwamba watu milioni 3 hawana chakula cha kutosha, huku milioni 2.5 wakitegemea tu chakula cha msaada.

Nalo Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la UNHCR limesema, linaongeza shughuli zake za kuwasaidia watu walolazimika kuhama makwao ndani mwa Syria. Bajeti ya UNCHR kwa ajili ya Syria sasa imeongezeka mara mbili zaidi na kuzidi dola milioni 41, na hizo ni tofauti na ufadhili wa misaada kwa wakimbizi wa Syria walioko nchi jirani katika kanda nzima ya Mashariki ya Kati. Adrian Edward ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)