Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu kwa watoto nchini Syria yakumbwa na utata siku za usoni:UNICEF

Elimu kwa watoto nchini Syria yakumbwa na utata siku za usoni:UNICEF

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa zaidi ya shule 2000 zimehabaribiwa nchini Syria. Linasema kuwa maelfu ya watoto hawataweza kurudi shuleni kwa mwaka mpya wa masomo unaoanza tarehe 16 mwezi Septemba.

UNICEF pia inasaidia kwenye ukarabati wa shule 64 kwa gharama ya dola milioni 8. Kuanza kwa masomo nchini Syria pia kumetatizwa kwa kuwa shule nyingi ndizo makao kwa wale waliohama makwao. Marixie Mercado kutoka UNICEF anasema kuwa karibu shule 603 zimetoa makao kwa familia zilizohama makwao.

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)