Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasambaza misada kwa raia wa Syria walio kwenye kambi nchini Uturuki

IOM yasambaza misada kwa raia wa Syria walio kwenye kambi nchini Uturuki

Chama cha mwezi mwekundu nchini Uturuki kwa niaba ya shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kimeendesha awamu ya pili ya usamabazaji wa misaada isiyokuwa chakula kwa raia wa Syria ambao kwa sasa wamepiga kambi kwenye maeneo ya Gaziantep, Hatay na Sanliurfa nchini Uturuki. Usambazaji wa misaada isiyokuwa chakula ni jambo muhimu hasa wakati huu wakimbizi wanapopata makao wengine wanapowasili nchini Uturuki bila chochote. Jumbe Omari Jumbe ni afisa wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)