Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlipuko wa Ebola bado ni tatizo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo:WHO

Mlipuko wa Ebola bado ni tatizo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo:WHO

Wizara ya afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaendelea kushirikiana na wadau wengine likiwemo shirika la afya duniani kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa homa ya ebola.

Kwa mujibu wa WHO hadi Septemba 3 mwaka huu jumla ya visa 28 vimebainika vikiwemo sita vya kukisiwa na vifo 14 kwenye wilaya ya Haut-Uélé jimbo la Orientale.

Visa hivyo na vifo vimetokea katika maeneo mawili, visa 18 ikiwemo vifo 11 katika eneo la Isiro na visa 19 ikiwemo vifo vitatu eneo la Vianda na vifo vya Isiri vinajumuisha wafanyakazi watatu wa afya. Alice Kariuki anaripoti.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)