Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bima ya afya ni mkombozi kwa watu maskini

Bima ya afya ni mkombozi kwa watu maskini

Kuwepo kwa mifumo ya bima za afya kunatajwa kwamba kunaweza kutoa mchango mkubwa ufikiaji wa usawa wa pamoja juu ya huduma za kiafya.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa katika nchi za Asia na Afrika unasema kuwa kuwepo kwa hali hiyo kutapunguza kiwango cha watu wanaolazimika kulipia huduma hizo pindi wanapozihitaji.

Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la shirika la afya ulimwenguni WHO unaonyesha kuwa nchi maskini ambazo zinaidadi kubwa ya watu  ndizo zinazopata shida kutokana na kiwango cha umaskini kuwa juu.

Unasema kuwa watu wengi wanaabiliwa na changamoto nyingi kupata huduma bora zakiafya tena katika wakati muafaka.