Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM, Kenya zakubaliana kuanzisha mashirikiano ya kusafirisha wafanya kazi vijana

IOM, Kenya zakubaliana kuanzisha mashirikiano ya kusafirisha wafanya kazi vijana

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM pamoja na serikali ya Kenya kwa pamoja wamekubaliana kuanzisha mashirikiano ya miaka minne ambayo yatashuhudia idadi kadhaa ya watu wenye ujuzi wa kufanya kazi wakisafirishwa katika mataifa ya nje.

Mpango huo utakapoanza kutekelezwa unakusudia kuwafaa zaidi vijana na kwa sasa inakisiwa kuwa kila mwaka kiasi cha vijana 6,000 watasafirishwa nje.

Serikali ya Kenya ndiyo inayogharimia mpango huo lakini kwa kupata msaada mwingine kutoka kwa mashirika mawili wahisani.

IOM lakini imepanga kuanzisha hatua ya utambuzi wa awali kwa wale watakaosafiri ikiwemo pia kuwafanyia tathmini za kiafya ili kuwarahisishia mambo pindi mpango huo utakapoanza kutekelezwa.