Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM na Japan wazindua mpango kuhusu usimamizi wa mpaka nchini Sudan Kusini

IOM na Japan wazindua mpango kuhusu usimamizi wa mpaka nchini Sudan Kusini

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na serikali ya Japan wametia sahihi makubaliano ya kuzindua mpango mpya wa kufanya kazi na serikali ya Sudan Kusini wa kuwa na kikosi cha polisi na kusimamia mipaka yake na kujenga vituo 16, katika ujenzi wa taasisi ya uhamiaji mjini Juba na kubuni mfumo wa mafunzo kuhusu usimamizi wa mipaka.

Mpango huo wa miaka miwili wa gharama ya dola milioni 5.4 unaofadhiliwa na serikali ya Japan utaisaidia Sudan Kusini kusimamia maeneo ya mipaka na kuchangia kuboreka kwa usalama wa kitaifa.