Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kundi la UM laitaka Tunisia kulinda mafanikio kwenye usawa na haki za binadamu kwa wanawake

Kundi la UM laitaka Tunisia kulinda mafanikio kwenye usawa na haki za binadamu kwa wanawake

Kundi la Umoja wa Mataifa linalohusika na masusla ya ubaguzi dhidi ya wanawake limetoa wito kwa serikali mpya ya Tunisia kuchukua kila hatua kulinda mafanikio yaliyopatikana nchini humo kuhusu usawa, kutokuwepo ubaguzi na haki za wanawake kuambatana na kanuni za kimataifa kuhusu haki za binadamu.

Watalaamu hao wamewapongeza viongozi nchini Tunisia ambao wamefanya jitihada za kuleta usawa kati ya wanawake na wanaume tangu nchi hiyo ipate uhuru. Hata hivyo kundi hilo lina wasi wasi kuhusu kipengee kimoja kwenye katiba kuhusu usawa na haki za wanawake huenda kikarudisha nyuma mafanikio yaliyopatikana kwa muda wa karibu miongo mitano iliyopita. Katika miaka ya hivi karibuni Tunisia imekuwa kwenye mstari wa mbele kupigania mabadiliko kwenye demokrasia na haki za binadamu. Tarehe 14 mwezi Januari mwaka 2011 Tunisia ilianza kushuhudia mabadiliko ya kisiasa na mwezi Disemba ilibuniwa serikali ya mpito.