Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sheria mpya ya EU kuhusu Uchafu wa Vifaa vya Komputa yaanza kutekelezwa:UNEP

Sheria mpya ya EU kuhusu Uchafu wa Vifaa vya Komputa yaanza kutekelezwa:UNEP

Jumuiya ya nchi za Ulaya imeweka kanuni mpya kuhusu mabaki ya vifaa vya elektroniki (yaani e-waste) ambazo zinatoa uwezo kwa nchi wanachama wa EU kukabiliana ipasavyo na uuzaji haramu wa mabaki kama hayo.

Sheria hiyo mpya pia inatazamia kuboresha viwango vya kurejesha mabaki ya vifaa vya elektroniki, na imetokana na aina mbalimbali za utafiti, ukiwemo Mkataba wa Basel.

Utafiti wa hivi karibuni ulotokana na mkataba wa Basel kuhusu mabaki ya elektroniki barani Afrika, umeonyesha mtiririko wa mabaki ya vifaa vya elekroniki unaoingia barani humo kutoka mataifa yaloendelea, yakiwemo wanachama wa EU, kwa ajili ya kurejeshwa au kutupwa kama taka.

Mkataba wa Basel unasimamiwa na Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP. Jason Nyakundi ana maelezo zaidi.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)