Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yakabiliana na Ebola nchini Uganda

WHO yakabiliana na Ebola nchini Uganda

Shirika la afya duniani WHO linashirikiana na wizara ya afya nchini Uganda na mashirika mengine kukabiliana na mkurupuko wa ugonjwa Ebola nchini humo. WHO inasema kuwa ilichukua hatua za mara moja kulipothibitishwa kisa cha kwanza cha ugonjwa wa Ebola mnamo tarehe 28 mwezi Julai mwaka huu.

Msemaji wa WHO Fadela Chaib anasema kuwa visa 23 vimeripotiwa vikiwemo vifo 16 lakini akaongeaza hakuna kisa chochote cha ugonjwa huo kilichoripotiwa hadi sasa. Ebola ni ugonjwa ambao huletwa na virusi vinavyosambaa kwa haraka na vilivyo hatari, vinaavyosambaa kupitia maji maji ya mwili.