Mashua zawasafirisha watu 2500 kutoka mjini Renk nchini Sudan Kusini kwenda makwao

10 Agosti 2012

Huku mashua zikiwa tayari zimeondoka mji wa Renk kwenye jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini zikiwasafirisha zaidi ya raia 2500 wa Sudan Kusini waliokwama kwenye mji huo kwa miezi kadha hatma ya watu wengine 16,000 haijulikani baada ya kuwepo uwezekano wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kusitisha oparesheni zake kutokana na ukosefu wa fedha.

Kutokana na kuwepo hali mbaya ya usalama kwenye mpaka na Sudan mapema mwaka huu na kuanza kwa msimu wa mvua wengi wa wanaorejea nchini Sudan Kusini wanaendelea kuingia nchini humo kupitia mji wa Renk wakisubiri kusafirishwa kwenda makwao. Afisa wa IOM Jumbe Omari Jumbe anafafanua zaidi.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud