Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amos atoa wito wa Misaada kwa wakimbizi wa DRC walio nchini Rwanda

Amos atoa wito wa Misaada kwa wakimbizi wa DRC walio nchini Rwanda

Mkuu wa masuala ya kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa Valerie Amos ameitembelea kambi ya Kigeme iliyo kusini mwa Rwanda ambapo zaidi wakimbizi 11,500 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamepewa hifadhi. Zaidi ya watu 20,000 wamevuka mpaka wakikimbia ghasia kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini nchini DRC.

Kwa sasa serikali ya Rwanda na shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR wanaongoza shughuli kwenye kambi hiyo huku mashirika ya Umoja wa Mataifa na yale yasiyokuwa ya kiserikali wakitoa huduma muhimu kama za maji , usafi , afya na chakula. Akiwa nchini Rwanda Bi Amos amekutana na Waziri Mkuu Pierre Habururemyi na Waziri wa mambo ya kigeni Louise Mushikiwabo mjini Kigali ambapo mazungumzo yao yaliangazia jitihada zinazofanywa katika utoaji wa misaada nchini DRC na Rwanda. Walijadili pia changamoto watoaji huduma za kibinadamu wanazokumbana nazo, na juhudi za kikanda za kuutanzua mizozo. Jens Laerke ni msemaji wa OCHA