Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko yanayoendelea Syria yanatia Hofu:UNSMIS Babacar

Machafuko yanayoendelea Syria yanatia Hofu:UNSMIS Babacar

Mkuu wa mpango wa uangalizi wa Umoja wa mataifa nchini Syria UNSMIS Luteni Jenerali Babacar Gaye akizungumzia hali ya machafuko yanayoendelea Aleppo nchini Syria amesema anatiwa hofu sana na hasa kwa kuzidi kuzorota kwa hali na athari zake kwa raia.

Gaye amezitaka pande zote husika katika machafuko ya Syria kuwalinda raia na kuheshimu wajibu wao chini ya sheria za kimataifa za haki za binadamu. Amezitaka pande hizo kuacha kuwashamblia raia na kutumia silaha nzitonzito.

Ametoa wito kwa pande zote kuchukua hatua za lazima ili kuanzisha majadiliano ambayo amesema ndio njia pekee ya kuondoa machungu yanayowakabili raia na kumaliza mgogoro wa taifa hilo la Mashariki ya Kati.