Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uongozi wa Somalia lazima kujitahidi Kuwalinda Waandishi Habari:Mahiga

Uongozi wa Somalia lazima kujitahidi Kuwalinda Waandishi Habari:Mahiga

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga ametoa wito kwa serikali ya mpito ya Somalia kuwalinda waandishi habari na kazi zao.

Mahiga amesema afosi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kisiasa ya Somalia UNPOS iko tayari kuisaidia serikali kukomesha ukatili na unyanyasaji dhidi ya waandishi na kumaliza mzunguko wa wahalifu kukwepa sheria.

Akizungumza Alhamisi mjini Moghadishu balozi Mahiga amesema licha ya ahadi zilizotolewa wameshuhudia juhudi kidogo sana za uchunguzi wa uhalifu uliotendewa dhidi ya wanahabari. Mahiga ametoa wito huo Alhamisi alipokuwa akilaani vikali mauaji ya mfanyakazi wa vyombo vya habari na mchekeshaji Abdi Malaq Jeylani almaarufu Marshale aliyeuawa Julai 31 nje ya nyumba yake mjini Moghadishu. Mahiga amesema karibu kila mwezi mwandishi habari anauawa na hili ni jambo lisilokubalika.