Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kituo cha haki za binadamu Tanzania chalaumu kuvunjwa kwa haki za binadamu

Kituo cha haki za binadamu Tanzania chalaumu kuvunjwa kwa haki za binadamu

Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania leo kimetangaza ripoti yake ya awali inayoangazia mwenendo wa haki za kibinadamu kwa nchi hii katika kipindi cha miezi sita iliyopita na kutaja kasoro kadhaa ikiwemo kushamiri kwa matukio ya ubakaji unawandama hasa wanawake na watoto wa shule pamoja na vyombo vya dola kuangukia kwenye lawama ya utumizi mabaya wa madaraka.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kwa mujibu wa ripoti ya kituo hicho, kiwango cha kuheshimiwa kwa haki za binadamu katika kipindi cha miezi sita iliyopita, siyo cha kutia matumaini na kwa ujumla wake kumeshuhudiwa hali ya kuyumba yumba kwa ustawi wa kibinadamu.

Akijadilia ripoti hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Dr Hellen Kijibisamba, amesema kuwa

Wakati vyombo vya dola vikiendelea kulaumiwa wa watetezi wa haki za binadamu kutokana na namna vinavyoshindwa kuwajibika, kadhali ustawi jumla wa makundi ya watu wanaoshika nafasi za usoni kupigania haki na usawa wa binadamu nao uko mashakani.

Kwa upande wa pili, ripoti hiyo imefichua mienendo na vitendo vya ubakaji vinavyowaandama hasa watoto wa shule na kina mama, huku Mkoa wa DSM, ukitaja kushika nafasi ya kwanza kwa kushamiri kwa vitendo hivyo.

Makundi ya kiharakati pamoja na vyombo vya habari tayari yameanza kuijadilia ripoti hiyo ya haki za binadamu.