Skip to main content

Baraza la Usalama lazitolea mwito Israel na Lebanon kuendelea na Majadiliano Kumaliza Mikwamo

Baraza la Usalama lazitolea mwito Israel na Lebanon kuendelea na Majadiliano Kumaliza Mikwamo

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea kuridhishwa kwake na hatua zinazopigwa kukwamua mkwaruzano wa mambo baina ya Israel na Lebanon ambazo zimeshindana kwa muda mrefu juu ya eneo linalojulikana ukanda wa Blue unaotenganisha mataifa hayo mawili.

Hata hivyo baraza hilo limezihimiza mataifa hayo kuendelea kupiga hatua zaidi ili kuyatafutua ufumbuzi baadhi ya maeneo yaliyosalia.

Katika taarifa yake kufuatia mkutano wake wa ndani, baraza hilo la usalama limezitolea mwito pande zote mbili kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na tume ya pande tatu ili kufikia shabaha ilitokusudiwa.