Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Awamu ya mwisho ya mazunguzmo ya Sahara Magharibi yakamilika mjini New York

Awamu ya mwisho ya mazunguzmo ya Sahara Magharibi yakamilika mjini New York

Awamu ya tano ya mazungumzo yanayoongozwa na Umoja wa Mataifa kuhusu mzozo wa Sahara Magharibi yamekamilika huku Morocco na eneo la la Frente Polisario wakikubaliana kuendelea na mazungumzo hayo mwezi Machi.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukihusika katika upatikanaji wa suluhu katika eneo la Sahara Magharibi tangu mwaka 1976 wakati kulipotokea mapigano kati ya Morocco na eneo la Frente Polisario kufuatia kukamilika kwa utawala wa kikoloni. Morocco imetoa mpango ya kulitawala eneo hilo wakati msimamo wa Frente Polisario ukiwa ni kwamba hatma ya eneo hilo iamuliwe kupitia kwa kura ya maoni . Ujumbe kutoka mataifa jirani ya Algeria na Mauritania ulihudhuria wakati wa ufunguzi na kukamilika kwa mazunguzzmo hayo yaliyochukua muda wa siku tatu yaliyoandaliwa kwa mwaliko wa mjumbe wa katibu mkuu katika eneo la Sahara Magharibi Christopher Ross.