Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaangazia huduma za HIV kwa wahamiaji katika mkutano wa kimataifa wa 19 kuhusu Ukimwi

IOM yaangazia huduma za HIV kwa wahamiaji katika mkutano wa kimataifa wa 19 kuhusu Ukimwi

Licha ya kauli za kisiasa kwenye viwango vya ngazi ya juu zaidi kuhusu kukabiliana na hatari ya kiafya na HIV kwa wahamiaji, watu hawa na jamii nyingine za kuhamahama bado wanashindwa kupata huduma za HIV katika mataifa mengi tu.

Hii ni kasoro ya afya ya umma ambayo inahitaji kushughulikiwa kwa dharura, hasa katika ulimwengu unaotegemea watu kuhama hama- limesema Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM, kabla ya mkutano wa kimataifa wa 19 kuhusu HIV na Ukimwi, unaoanza mwishoni mwa wiki mjini Washington Marekani.

Shirika la IOM limesema, sasa ndio wakati wa kila nchi kuchukua hatua ya kijasiri, na kuhakikisha kujitolea katika kulinda haki ya kila mtu ya afya. Katika mkutano wa Washington, IOM itashiriki katika baadhi ya mambo, na kutoa ushauri kuhusu jinsi ya kukabiliana na hatari za HIV zinazowakumba wahamiaji au jamii za kuhamahama.