Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mipaka Duni na Taasisi hafifu inachagia Ulanguzi wa Madawa ya Kulevya na uhalifu Afrika Magharibi:UM

Mipaka Duni na Taasisi hafifu inachagia Ulanguzi wa Madawa ya Kulevya na uhalifu Afrika Magharibi:UM

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika ya magharibi, Said Djinnit amesema mipaka ya mataifa ya Afrika Magharibi haijadhibitiwa vyema, na hivyo, pamoja na taasisi hafifu za kiserikali, inaruhusu biashara katika madawa haramu kuenea katika eneo hilo na mataifa ya Amerika ya Kusini.

Amesema pia katika miaka ya hivi karibuni, matumizi ya madawa ya kulevya katika mataifa ya Afrika Magharibi pia yameongezeka, jambo ambalo amesema linatia hofu.

Ameongeza kuwa madawa pia yanaongeza hatari za kiafya na kiusalama, hasa kwa sababu ulanguzi wa madawa ya kulevya yanachagiza biashara katika silaha pamoja, usafirishaji haramu wa watu na ufisadi.