Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wakosa huduma muhimu wakati mgogoro ukiendelea CAR

Watoto wakosa huduma muhimu wakati mgogoro ukiendelea CAR

Maelfu ya watoto nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wameachwa bila hudumu muhimu za kutosha wakati waasi wakisonga mbele na kuelekea mji mkuu Bangui limesema shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Kwa mujibu wa shirika hilo maeneo yanayodhibitiwa na waasi huduma za afya zimeathirika vibaya huku shule nyingi zikiwa zimefungwa au kuchukuliwa na makundi yenye silaha.

UNICEF inasema takribani watoto 14,000 wanatarajiwa kukabiliwa na maradhi ya utapia mlo kufuatia kuporwa na kufungwa kwa vituo vya lishe. Kwa mujibu wa msemaji wa UNICEF Marixie Mercado shika limepokea taarifa za uhakika kwamba makundi ya waasi na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali wamekuwa wakiwafunza na kuwaingiza watoto kwenye majeshi yao.

Ameongeza kuwa watoto hao wengi wamepoteza nyumba zao , wametenganishwa na familia zao au awali walishirikishwa katika makundi yenye silaha.UNICEF inakadiria kwamba watoto 2500 wavulana kwa wasichana wamekuwa wakijihusisha na makundi yenye silaha.