Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mswada wa Azimio Kuhusu Syria wakataliwa

Mswada wa Azimio Kuhusu Syria wakataliwa

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limeshindwa kuafikiana kuhusu Mswada wa azimio lenye lengo la kukomesha umwagaji damu nchini Syria. Azimio hilo limeungwa mkono na nchi kumi na moja wanachama wa Baraza hilo, lakini halijapitishwa kwa sababu limekataliwa na Urusi na Uchina, ambao ni wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama, na wenye ushawishi mkubwa. Wanachama wawili wa Baraza hilo hawakuegemea upande wowote.

Azimio hilo lilinuia kubadilisha mazingira ya ghasia yaliyopo sasa katika nchi ya Syria, ili kuwezesha utekelezaji wa mpango wenye vipengee sita wa mwakilishi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu, Kofi Annan.

Balozi wa Urusi kwenye Umoja wa Bataifa alikuwa na haya ya kusema:

(RUSSIA)

Naye balozi wa Uingereza alikuwa na haya ya kusema

(UK CLIP)

Awali, Bwana Annan alikuwa ametoa wito kwa wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa waungane kwa ajili ya kuchukuwa hatua inayofaa kwa ajili ya Syria, katika mkutano huo wa Baraza la Usalama.