Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS yapongeza Uongozi wa Shirika la AWA

UNAIDS yapongeza Uongozi wa Shirika la AWA

Mkurugenzi mkuu wa shirika la kupambana na ugonjwa wa ukimwi la Umoja wa Mataifa UNAIDS Michel Sidibe amelipongeza shirika la kupambana ugonjwa wa ukimwi barani Afrika la AIDS Watch Afrika (AWA) na kulitaja kuwa kiongozi katika vita dhidi ya ukimwi barani Afrika.

Akihutubia zaidi ya maafisa 20 wa ngazi za juu mjini Addis Ababa nchini Ethiopia Sidibe amesema kuwa shirika la AWA linahitajika zaidi barani Afrika sasa kwenye vita dhidi ya ukimwi, kifua kikuu,, malaria na chanagamoto zingine za kiafya. Kwa upande wake mwenyekiti wa AWA na rais wa Benin Dr Boni Yayi amesema kuwa kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi barani na magonjwa mengine kama wa kifua kikuu na malaria kutahitaji kujitolea na uongozi mwema.