Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufisadi Unazuia Mataifa Kuendelea:Ban

Ufisadi Unazuia Mataifa Kuendelea:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema kuwa ufisadi ni kizuizi kikubwa cha maendeleo katika mataifa mengi, na unafaa kukabiliwa kwa uwazi na uajibikaji. Akilihutubia jopo la ngazi ya juu kuhusu uwajibikaji, uwazi na maendeleo endelevu, Bwana Ban amesema tatizo la ufisadi linawaathiri zaidi watu wenye uwezo mdogo, kwani wanalazimika kulipa rushwa ili kupata huduma ambazo wana haki kupata, kama vile kupata leseni ya udreva, kupata matibabu, kutendewa wema na polisi au kupata haki kotini. Amesema ufisadi kama huo huchangia uhalifu, hudhoofisha demokrasia na kufanya umma kutokuwa na imani na serikali.

Amesema amani, maendeleo au haki za binadam haziwezi kushamiri katika mazingira ya ufisadi, na kwamba athari za ufisadi ni kubwa hata zaidi katika jamii zenye uongozi hafifu wa kisheria, na taasisi duni, na kuwa athari zake kwa maendeleo ni za moja kwa moja na mbaya hata zaidi. Ametoa mfano kuwa, mwaka uliopita pekee, ufisadi ulizuia asilimia 30 ya fedha za msaada wa maendeleo kufikia walengwa. Amesema hii inamaanisha daraja, shule, na hospitali hazikujengwa, na watu wanaishi bila faida za huduma hizi.

Ametoa wito ufanywe ushirikiano baina ya sekta za kibinafsi, mashirika ya umma, elimu, vyombo vya habari, wanawake na vijana ili kujenga desturi ya heshima