Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kiwango wastani cha bei ya chakula chashuka tena:FAO

Kiwango wastani cha bei ya chakula chashuka tena:FAO

Kiwango wastani cha bei ya chakula kimeshuka kwa mwezi wa tatu mfululizo mnamo mwezi Juni mwaka 2012. Kiwango hicho kimeshuka kwa kwa pointi 4, ambazo ni asilimia 1.8 kutoka mwezi Mei, na hivyo kufikia kiwango cha chini zaidi cha kipimo wastani cha bei ya chakula tangu mwezi Septemba 2010.

Kiwango wastani cha kipimo cha bei ya chakula sasa kimeshuka kwa asilimia 15.4, chini ya kilivyokuwa mwezi Februari mwaka 2011.

Bei ya wastani ya aina zote za bidhaa ilishuka na kuwa chini ya ilivyokuwa mwezi Mei, kiwango kikubwa zaidi cha kupungua huko kikionekana katika bidhaa za mafuta ya kupikia. George Njogopa anaripoti