Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka kodi kuchangisha dola bilioni 400 kufadhili mahitaji ya maendeleo

UM wataka kodi kuchangisha dola bilioni 400 kufadhili mahitaji ya maendeleo

Umoja wa Mataifa unapendekeza kodi ya kimataifa, na ubunifu wa njia zingine za kupata fedha, ili kuchangisha dola bilioni 400 kila mwaka kwa ajili ya kufadhili maendeleo, na changamoto zingine zinazoikabili dunia, kama vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Mapendekezo hayo yamo kwenye ripoti ya mwaka huu ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo iliyotokana na utafiti wa masuala ya jamii na uchumi kwa mwaka 2012.

Ripoti hiyo ya maendeleo mapya katika masuala ya fedha imezinduliwa Alhamisi asubuhi, na Umoja wa mataifa umesema, katika wakati huu wa msukosuko mkubwa wa fedha nchi nyingi wafadhili wamepunguza msaada wao wa maendeleo. Mwandishi mkuu wa utafiti huo Rob Voss amesema nchi wafadhili hawajamaliza kutimiza ahadi zao za msaada, na maendeleo yameshuka mwaka jana kwa sababu wengi wamepunguza bajeti zao, na kulifanya pengo kuwa dola bilioni 167.