Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi na Ulanguzi wa Madawa ya Kulevya kunachangia Uhalifu

Matumizi na Ulanguzi wa Madawa ya Kulevya kunachangia Uhalifu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-Ki-Moon, amesema kwamba madawa ya kulevya na mitandao husika ya uhalifu inachangia kwa kiasi kikubwa ukiukaji wa sheria. Katika hotuba yake kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwenye siku ya kimataifa dhidi ya matumizi na ulanguzi wa madawa ya kulevya, Bwana Ban amesema mabilioni ya fedha zinazotokana na ulanguzi madawa ya kulevya zinachangia vitendo vya kigaidi, na kuwezesha kutendeka aina nyingine za uhalifu, ukiwemo usambazaji wa silaha na usafirishaji haramu wa watu.

Amesema kutochukuliwa hatua za kisheria wanaotenda vitendo hivi, kunawaongezea watu wa kawaida uoga na kuwafanya wakose kuwa na imani katika serikali zao.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)