Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya UNMISS yataka Wahusika wa Ghasia Jonglei Wawajibishwe

Ripoti ya UNMISS yataka Wahusika wa Ghasia Jonglei Wawajibishwe

Wawakilishi wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMISS, wametoa ripoti mpya leo ya uchunguzi wa kina uliofanywa kuhusu ghasia za kikabila kwenye jimbo la Jonglei, ambazo zilisababisha vifo vya mamia ya watu mwaka jana na mapema mwaka huu.

Ripoti hiyo, yenye kichwa: Visa vya ghasia za kikabila katika jimbo la Jonglei, ripoti hiyo ya kurasa 45 inajumuisha visa vya uhalifu na ukiukaji wa haki za binadam vilivyotendeka wakati wa ghasia hizo, na kupendekeza njia tisa za kuepukana na ghasia kama hizo siku zijazo. Jason Nyakundi anaripoti

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)