Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UM yasifu juhudi za kupambana na lishe duni

Mashirika ya UM yasifu juhudi za kupambana na lishe duni

Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya WFP, UNICEF, WHO na FAO yameusifu mchakato wa kuzuia lishe duni miongoni mwa watoto, yaani REACH, kama msingi wa malengo ya maendeleo endelevu.

Mashirika hayo kwa pamoja yamesema, mkutano wa Rio + 20 unatoa fursa kwa muafaka kuhusu siku za baadaye zinazotakiwa. Yamesema ni siku ambazo zitategemea ari ya kimataifa kuhusu maendeleo endelevu ya miaka ijayo, ambayo yanaweza kufikiwa kwa kuunga mkono michakato inayoweka msingi thabiti wa kuyafikia malengo hayo.

Mashirika hayo yameelezea kujitolea kuunga mkono juhudi za mchakato wa REACH, unaolenga kuzuia njaa na lishe duni miongoni mwa watoto. Jason Nyakundi anaripoti

(RIPOTI YA JASON NYAKNDI)