Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Wakimbizi 2012 - Msaada zaidi wahitajika

Siku ya Wakimbizi 2012 - Msaada zaidi wahitajika

“Wakimbizi hawana uhuru wa kuchagua. Unao wewe.” Hayo ndiyo maudhui ya Siku ya Wakimbizi Duniani, ambayo huadhimishwa kila tarehe 20 Juni.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, kila dakika moja ipitayo, watu wanane huacha kila kitu wanachokimiliki na kukimbilia usalama wao kwa sababu ya vita, mateso au ugaidi.

Kwa mwaka wa tano mfululizo, kuna zaidi ya watu milioni 42, ambao wamelazimika kuhama makwao kote duniani. Katika ujumbe wake kwenye siku hii ya wakimbizi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, amesema idadi hii inawakilisha zaidi ya takwimu tu.

Amesema, hawa ni watu binafsi, au jamaa ambazo maisha yao yamepinduliwa, jamii zao kuangamizwa, na ambao hawajui hali yao ya baadaye. Amesema, licha ya kuwa na uhaba wa fedha kila mahali, hatuna budi kuwasaidia watu waliomo katika hali hii ya ukiwa. Ametoa wito kwa kila kila mtu kufanya juhudi ili kuchagiza ari na uongozi wa kisiasa kuzuia na kukomesha migogoro ambayo huchangia mtiririko wa wakimbizi. Anjelina Jolie ni balozi mwema wa UNHCR

(SAUTI YA ANJELINA JOLIE)

Nao wakimbizi wa ndani na nje Afrika ya Mashariki wana maoni gani kuhsu siku hii?

(MAONI YA AFRIKA MASHARIKI)