Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwa mkimbizi sio chaguo ni shuruti:Jolie

Kuwa mkimbizi sio chaguo ni shuruti:Jolie

Balozi wa hisani wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR Angelina Jolie anaamini kuwa kumlazimisha mtu mmoja kwenda ukimbizini ni kitendo kinachokusanya watu wengi.

Katika ujumbe wake katika siku ya kuadhimisha siku ya wakimbizi duniani, balozi huyo amesema kuwa kwa mtu mmoja kulazimishwa kwenda ukimbizoni ni jambo lisilovumilika na linachukua sura kubwa.

Amesema kuwa tatizo la ukimbizi linaendelea kumea mizizi ,likiwaandama maelfu ya wananchi jambo ambalo linakwaza ustawi wa kijamii.

Takwimu za hivi sasa zinaonyesha kuwa katika kipindi miaka michache iliyopita, zaidi ya watu milioni 4.3 wameangukia kwenye maisha ya ukimbizi.Lakini pia kuna kiasi cha wakimbizi wa kiafhganistan milioni 2.7 wanaendelea kutabika.