Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OCHA yatangaza ombi mpya la msaada kwa eneo la Sahel

OCHA yatangaza ombi mpya la msaada kwa eneo la Sahel

Umoja wa Mataifa pamoja na washirika wengine wa kutoa huduma za kibinadamu hii leo wametoa wito mpya wa misaada ya kuwasaiadia watu wa Sahel magharibi mwa Afrika.

Wito huo wa pamoja ambao ni wa dola bilioni 1.6 utagharamia huduma za chakula , afya , usafi na usaidizi mwingine ambao utatolewa kwa watu milioni 18.7.

Wito mpya ulitolewa kusaidia mataifa ya Burkina Faso,  Mali, Mauritania, Chad na Niger huku Cameroon na Gambia pia zikitajwa kuwa baadhi ya nchi zinazohitaji misaada. David Gressly ni mtatibu wa shirika la OCHA eneo la Sahel.

(SAUTI YA DAVID GRESSLY)