IOM yaendelea kuahamisha wakimbizi wa Sudan Kusini

18 Juni 2012

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeanzisha shughuli ya kuwahamisha wakimbizi kutoka kituo cha Al Damazin kilicho kwenye eneo la magharibi kati ya mpaka wa Ethiopia na Sudan kwenda kambi mpya iliyo eneo la Benishangul Gumuz kaskazini magharibi mwa Ethiopia.

Uamuzi wa kuhamisha wakimbizi hao ulifanywa baada ya kituo hicho ambacho kina uwezo wa kuwahifadhi watu 14,000 kufurika.

Mapigano yaliyoanza kushuhudiwa mwezi Septemba mwaka 2011 kati ya wanajeshi wa Sudan na kundi la kaskazini la Sudan people Liberation Movement (SPLM-N) kwenye jimbo la Blue Nile yamesababisha kuhama kwa maelfu ya watu wanaovuka mpaka na kuingia nchini Ethiopia kukimbilia usalama. Joshua mmali amezungumza na Jumbe Omari Jumbe ambaye ni afisa wa IOM.

(MAHOJIANO NA  JUMBE OMARI JUMBE)