Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa fedha wahatarisha operesheni Mali:UNHCR

Ukosefu wa fedha wahatarisha operesheni Mali:UNHCR

Ukosefu wa fedha unatajwa kutishia jitihada za shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR za kusaidia zaidi ya watu 300,000 nchini Mali waliolazimika kuhama makwao kutokana na mapigano na ukosefu wa usalama kaskazini mwa nchi.

UNHCR inasema kuwa hadi sasa imepokea asilimia 13 tu na dola milioni 153.7 zinazohitajika kuwasaidia raia waliohama makwao ndani na nje mwa nchi yaohuku watu zaidi wakindelea kukimbia mapigano. George Njogopa na anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)