Maendeleo endelevu hayawezekani bila kuheshimu haki za binadamu-asema Pillay

Maendeleo endelevu hayawezekani bila kuheshimu haki za binadamu-asema Pillay

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa Navi Pillay, amesema kuwa maendeleo endelevu hayawezi kuwepo bila kuheshimu haki za binadamu. Bi Pillay amesema haya kabla ya mazungumzo kuhusu mswada kuhusu matokeo ya mkutano wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu, Rio+20.

Bi Pillay atahudhuria mkutano huo wiki ijayo, ili kutoa shinikizo kwa viongozi kuhusu haja ya kujumuisha haki za binadamu katika mkataba wa matokeo ya mkutano huo.

Amesema haki za binadamu na maendeleo endelevu vinauiana sambamba, na bila njia wazi za kulinda haki za binadamu, sera zenye lengo la kulinda mazingira au kufanya maendeleo zinaweza kuwa na athari mbaya kwa haki za watu na hali yao ya maisha.